Mapendekezo ya tafsiri: Orodha kulingana na mada na zilizoainishwa na Jumuiya/Jinsi ya kutumia nduni
Mwongozo ufuatao utasaidia wachangiaji na waandaaji wa kampeni kutumia sifa za mapendekezo ya tafsiri katika zana ya kutafsiri Maudhui.
Jinsi ya kufikia zana ya Kutafsiri Maudhui (CX) kwenye simu ya mkononi
CX kwenye simu ya mkononi (pia inaitwa Tafsiri ya Sehemu) inaweza kufikiwa kupitia njia zifuatazo:
- Chaguo 1: Kiteuzi cha "Lugha" unapofungua makala ya Wikipedia kama this one, andika lugha unayotaka kutafsiri katika kisanduku cha kutafutia na ubofye kitufe cha "Andika tafsiri mpya" ili kufikia zana ya kutafsiri Maudhui kwenye simu ya mkononi, kama inavyoonyeshwa hapa chini.

- Chaguo 2: Kitufe cha "Tafsiri", kilichofikiwa kutoka kwa ikoni ya "Changia" inayopatikana katika menyu kunjuzi (hatua hii inapatikana kwa akaunti zisizo na michango katika Wiki ambapo sehemu ya "Changia" imewezeshwa).

Mwongozo wa uteuzi wa mada na Mikusanyiko
Jinsi ya kuvinjari aina za vichujio | |
---|---|
Aina ya kichujio ya “Kwa Ajili Yako”' hutoa mapendekezo kulingana na historia ya uhariri.
Aina ya kichujio ya “Maarufu” hutoa mapendekezo ambapo hakuna historia ya awali ya kuhariri. |
![]() |
Kichujio cha “...Zaidi” huruhusu mtu kuvinjari na kutazama lebo tofauti za mada. | ![]() |
2. Jinsi ya kuvinjari lebo za mada | |
Uteuzi mmoja wa mada kutoka kwa
Kichujio cha "...Zaidi", huonyesha mapendekezo ya tafsiri yanayohusiana na mada iliyochaguliwa. Kwa mfano, uteuzi wa Sanaa unaonyesha mapendekezo ya tafsiri yanayohusiana na Sanaa, kwa njia hiyo hiyo, uteuzi mmoja wa Mchezo utaonyesha mapendekezo ya tafsiri yanayohusiana na Michezo. Chini ni kielezo kinachoonyesha jinsi ya kubadilisha mada. |
![]() |
3. Jinsi ya kuvinjari lebo za "Mikusanyiko" na "Mikusanyiko Yote" | |
Uteuzi wa Makala Muhimu huleta mapendekezo ya tafsiri yanayohusiana na makala muhimu.
Uteuzi wa Mikusanyiko Yote huleta mapendekezo ya tafsiri yanayohusiana na mikusanyiko yote iliyopo (Pages including a page collection). |
![]() |
4. Jinsi ya kuongeza alama ya mkusanyiko kwenye kampeni/kurasa za wiki kwenye Meta | |
Mara ukurasa wa Meta wa kampeni/mradi wa wiki unapoorodheshwa na makala inayohitaji tafsiri, fuata hatua zilizo hapa chini ili kuongeza alama ya mkusanyiko wa ukurasa:
Upe mfumo muda usiozidi saa 1 ili orodha ionekane kwenye zana ya simu ya mkononi ya CX. |
![]() |