Jump to content

Msaada: Vichujio vipya vya uhakiki wa uhariri

From mediawiki.org
This page is a translated version of the page Help:New filters for edit review and the translation is 94% complete.
PD Kumbuka: ukifanya mabadiliko kwenye ukurasa huu, umekubali kutoa mchango wako chini ya kifungu CC0. Tazama Kurasa za Msaada wa Kikoa cha Umma kwa habari zaidi. PD

Vichujio Vipya vya Uhakiki wa Uhariri vinaongeza vichujio vipya na zana zingine pamoja na kiolesura cha uchujaji kwa Special:RecentChanges na Special:RecentChangesLinked (awali).

Zana hizi huwasaidia wakaguzi kulenga juhudi zao vyema na kuwa na ufanisi zaidi. Pia zinaweza kuwanufaisha hasa wachangiaji wapya, ambao wanahitaji mchakato wa uhakiki wa uhariri wenye msaada zaidi, kulingana na utafiti.

Ili kujifunza kuhusu sehemu za kiolesura kilichoboreshwa, tembelea muhtasari wa haraka. Ili kujifunza jinsi ya kutumia vipengele vya hali ya juu vinavyotolewa, chunguza kurasa zilizoelezwa hapa chini.

Usambazaji wa kipengele hiki ulianza Machi 2017. Kipengele cha “Vichujio vipya vya uhakiki wa uhariri” hakipatikani kwenye simu.

Kazi kuu

Uchujaji
Ukurasa huu unaeleza jinsi kiolesura kilichoboreshwa cha uchujaji kinavyofanya kazi na jinsi ya kufaidika zaidi na zana mpya.
Kuweka Matokeo Kwa Udhihiri
Zana za Kuweka Matokeo Kwa Udhihiri zinazobainishwa na mtumiaji hukuruhusu kutumia rangi ili kusisitiza uhariri unaokuvutia zaidi. Vipengele na mbinu zilizoelezwa kwenye ukurasa huu vitakusaidia kufanya matokeo ya Mabadiliko ya Hivi Karibuni yawe na maana zaidi.
Vichujio vya Ubora na Nia
"Vichujio vipya vya uhakiki wa uhariri" vinaanzisha makundi mawili ya vichujio—Ubora wa Michango na Nia ya Mtumiaji—ambayo yanaendeshwa na ujifunzaji wa mashine na hufanya kazi kwa njia tofauti na vichujio vingine. Zinatoa utabiri wa uwezekano kuhusu ikiwa uhariri una uwezekano wa kuwa na matatizo na ikiwa mtumiaji aliyefanya uhariri huo alikuwa akitenda kwa nia njema. Kujua kidogo kuhusu jinsi zana hizi za kipekee zinavyofanya kazi kutakusaidia kuzitumia kwa ufanisi zaidi.
Alamisho
Hifadhi na urejeshe vichujio vyako unavyopenda. You can also set the default filter.
Masasisho ya Moja kwa Moja
Matokeo yaliyochujwa husasishwa mara kwa mara.


Kuzima Vichujio

Watumiaji wanaozima JavaScript katika kivinjari chao, au wanaozima vichujio katika mapendeleo yao ya mtumiaji wataona kiolesura kisicho na JavaScript. RecentChanges au RecentChangesLinked zitapakia bila kazi kuu zilizoelezwa hapo juu.

Tazama pia

Maswali Yanayoulizwa Mara Kwa Mara
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
Ukurasa wa maoni
Majadiliano yanayoendelea na maoni yaliyotolewa na watumiaji.

Rasilimali nyingine